Got a TV Licence?

You need one to watch live TV on any channel or device, and BBC programmes on iPlayer. It’s the law.

Find out more
I don’t have a TV Licence.

Habari za moja kwa moja

Na Ambia Hirsi na Dinah Gahamanyi

time_stated_uk

  1. Na mpaka hapo ndio tunafikia mwisho wa matangazo yetu ya moja kwa moja kwa leo, tukutane tena hapo kesho.

  2. Burkina Faso yawafukuza wanadiplomasia wa Ufaransa

    g
    Image caption: Kiongozi wa kijeshi wa Burkinafaso Capt Ibrahim Traoré amekata uhusiano na Ufaransa na kuielekezaa Burkina Faso katika uhusiano na Urusi

    Kiongozi wa Junta Capt Ibrahim Traoré amekata uhusiano na Ufaransa na kuelekea Burkina Faso kuelekea Urusi

    Burkina Faso imewafukuza wanadiplomasia watatu wa Ufaransa kwa kujihusisha na "shughuli za uasi", wizara ya mambo ya nje ya Burkina Faso ilisema katika waraka wake kwa Ufaransa.

    Waraka huo uliotolewa tarehe 16 Aprili haukufichua aina ya shughuli hizo.

    Wanadiplomasia hao, ambao ni pamoja na washauri wawili wa kisiasa katika ubalozi wa Ufaransa huko Ouagadougou, wametakiwa "kuondoka katika eneo la Burkina Faso ndani ya saa 48 zijazo", ilani hiyo iliongeza.

    Uhusiano kati ya Burkina Faso na ukoloni wake wa zamani Ufaransa umedorora tangu Kapteni Ibrahim Traoré achukue mamlaka katika mapinduzi ya Septemba 2022.

    Kiongozi huyo wa kijeshi wa Burkina Faso amekuwa akiegemea zaidi upande wa Urusi, na kusitisha uhusiano wake wa karibu na mkoloni wa zamani Ufaransa.

    Chini ya utawala wake, wanadiplomasia kadhaa wa Ufaransa wamefukuzwa na kambi ya kijeshi ya Ufaransa nchini humo kufungwa.

  3. Ajali ya helikopta ya kijeshi Kenya – tunachojua

    Maelezo kuhusu ajali ya helikopta ya kijeshi ya Kenya bado yanaendelea kutolewa, lakini hapa kuna baadhi ya kile tunachojua:

    • Helikopta ya kijeshi imeanguka kwenye mpaka wa kaunti za Pokot Magharibi na Elgeyo Marakwet katika Bonde la Ufa nchini Kenya.
    • Msemaji wa serikali Isaac Mwaura amethibitisha kuwa kumetokea ajali lakini amewataka Wakenya kuwa watulivu na kuepuka uvumi.
    • Hakujakuwa na uthibitisho rasmi juu ya nani alikuwa kwenye bodi
    • Vyombo vya habari vya ndani vinaripoti kuwa maafisa wakuu wa jeshi walikuwa kwenye helikopta hiyo
    • Timu za uokoaji zimetumwa kwenye eneo la ajali ili kutoa usaidizi na kutathmini hali hiyo
    • Wakenya wanasubiri taarifa kutoka kwa Rais William Ruto wakati wowote
  4. Mshindi wa rekodi ya dunia Kiptum kupewa heshima katika mbio za London Marathon

    g
    Image caption: Kelvin Kiptum alivunja rekodi ya kozi hiyo aliposhinda London Marathon mwaka jana

    Mshindi wa rekodi ya dunia ya mbio za marathon, Mkenya Kelvin Kiptum, ataenziwa katika mbio za London Marathon siku ya Jumapili.

    Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alifariki pamoja na kocha wake, Gervais Hakizimana wa Rwanda, katika ajali ya gari magharibi mwa Kenya mwezi Februari.

    Kiptum alipangiwa kushiriki katika mbio za London Marathon za mwaka huu, ambapo alikuwa akitazamia kushinda kwa mwaka wa pili mfululizo.

    Tukio hilo litaanza kwa heshima kwa Kiptum.

    "Tutakachokuwa tukifanya... ni kumsherehekea," mkurugenzi wa hafla Hugh Brasher alisema katika mahojiano na BBC Sport.

    "Na tutakuwa tukitoa hotuba kabla na kuwataka washiriki wote kushiriki katika sekunde 30 za kumshangilia Kelvin - kwa maisha ambayo hatukuwa tunamjua, kwa mtu ambaye hatumjui, lakini pia kwa kile alichokipata, mafanikio, kwa mtu aliyekuwa na kwa kifo cha kusikitisha kilichotokea mapema mwaka huu."

    Kiptum alikuwa ameweka rekodi katika mbio zote tatu za marathoni alizokimbia katika maisha yake ya muda mfupi.

    Aliweka rekodi katika mbio za mwisho za London Marathon.

    Muda mfupi baadaye, alikimbia mbio za marathon za kasi zaidi katika historia huko Chicago, akiweka rekodi ya kukimbia kwa 2:00.35.

    Kiptum pia aliweka rekodi ya kukimb ia mbio za haraka zaidi za marathon katika mbio zake za kwanza za marathon huko Valencia.

    Mbio za Rotterdam Marathon, ambapo Kiptum alipanga kukimbia, pia zilitoa heshima kwake Jumapili iliyopita.

    Washiriki, akiwemo mke wa Kiptum Asenath Rotich, walishiriki katika tukio la kukaa kimya kwa dakika moja kwa heshima yake.

  5. Habari za hivi pundeWatu watano wamefariki katika ajali ya ndege ya kijeshi Kenya - ripoti

    Kituo cha runinga cha Kenya NTV kinaripoti kuwa kulingana na msemaji wa polisi watu watano kati ya waliokuwa kwenye helikopta ya kijeshi ambayo imeanguka wamefariki.

    Kulikuwa na watu watatu walionusurika, polisi wanaripotiwa kusema.

    Shirika la habari la Reuters pia linaripoti takwimu hizo zikinukuu chanzo cha polisi kisichojulikana.

    Watu watatu walionusurika wanatibiwa hospitalini, inaongeza.

  6. Habari za hivi pundeWakenya wametakiwa kuwa watulivu baada ya habari za kuanguka kwa helikopta

    Msemaji wa serikali ya Kenya Isaac Mwaura amewataka Wakenya "kuwa watulivu na kuepuka uvumi wowote katika wakati huu mgumu".

    Ujumbe wake kwa X unafuatia habari kwamba helikopta ya kijeshi imeanguka na ripoti kwamba baadhi ya maafisa wakuu walikuwa ndani.

    "Mawasiliano rasmi kuhusu Ajali ya Ndege ya Kijeshi yatatolewa hivi karibuni," msemaji huyo alisema.

  7. Habari za hivi pundeHelikopta ya jeshi la Kenya yaanguka

    Helikopta ya jeshi la Kenya yaanguka Helikopta ya Jeshi la Ulinzi nchini Kenya imeanguka muda mfupi baada ya kupaa huku kukiwa na ripoti za maafa .

    Kituo cha habari cha Citizen TV kinaripoti kwamba mkuu wa jeshi Jenerali Francis Ogolla alikuwa miongoni mwa waliokuwa wakisafiri ndani ya ndege hiyo.

    Msemaji wa Ikulu Hussein Mohammed amesema rais William Ruto ameitisha mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Kitaifa katika Ikulu ya Nairobi jioni ya leo kufuatia ajali ya helikopta ya Jeshi la Kenya alasiri ya leo katika Kaunti ya Elgeyo-Marakwet.

  8. Uwanja wa ndege wa Dubai wafunguliwa tena baada ya UAE kukumbwa na mvua kubwa

    v
    Image caption: Maafisa waliwataka watu kusafiri hadi kwenye uwanja wa ndege ikiwa tu wamethibitisha kuhifadhi

    Shughuli katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dubai bado zimetatizika pakubwa baada ya mvua kubwa kunyesha katika Umoja wa Falme za Kiarabu na nchi jirani.

    Dhoruba hiyo kali iliipiga UAE siku ya Jumanne, na kusababisha barabara maji kwabarabara na sehemu za uwanja wa ndege wa kimataifa wenye shughuli nyingi.

    Mafuriko makubwa sasa yameua watu 20 nchini Oman na mmoja katika UAE.

    Baadhi ya safari za ndege za ndani zimeanza tena Alhamisi, lakini katika uwanja mzima wa ndege wa kimataifa wa Dubai, kituo kikuu cha usafiri, kinatatizika kufanya kazi.

    Maafisa wamamlaka katika uwanja huo wa ndege wa pili kwa shughuli nyingi zaidi duniani siku ya Alhamisi walisema kwamba walikuwa wameanza kupokea safari za ndege zinazoingia ndani katika Terminal 1, zinazotumiwa na wachukuzi wa kigeni, lakini safari za nje zinmeendelea kuchelewa.

  9. Lewis Hamilton: Nina mpango wa kukimbia hadi umri wa miaka ya 40

    g
    Image caption: Lewis Hamilton alicheza kwa mara ya kwanza kwenye Formula 1 mwaka wa 2007, huku mbio za kwanza za Fernando Alonso katika mchezo huo zikiwa mwaka 2001.

    Lewis Hamilton anasema ataungana na mpinzani wake wa zamani Fernando Alonso katika mbio za Formula 1 "hadi miaka ya 40".

    Mkataba mpya wa Alonso wa Aston Martin utamweka kwenye F1 hadi angalau 2026, baada ya kutimiza miaka 45.

    Hamilton atakuwa na umri wa miaka 40 mwaka ujao atakapoanza kazi yake na Ferrari, ambayo ni ni makubaliano ya miaka miwili.

    "Mimi sio dereva mzee zaidi hapa. Nitaendesha magari kwa muda mrefu sana kwa hivyo ni vizuri Alonso bado yuko," Hamilton alisema.

    "Fernando ni mmoja wa madereva bora ambao tumekuwa nao katika mchezo huo kwa hivyo kwa yeye kuendelea kuwa hapa na kuendelea kuwa na matokeo ambayo alikuwa nayo inaonyesha kile kinachowezekana."

    Dereva wa McLaren, Lando Norris alisema mafanikio ya Alonso katika kushindana kwa muda mrefu katika kiwango cha juu katika Formula 1 huenda yasionekane tena.

    "Yeye ni mmoja wa vijana wa zamani zaidi kushindana juu katika mchezo wowote.” alisema Norris.

    Norris, ambaye ako na timu ya McLaren, alisema "anaheshimu sana" uwezo wa Alonso kuendelea kufanya kiwango cha juu kwa muda mrefu.

    Kujitolea kwa Alonso na muda mrefu katika F1 kunaweka kiwango kipya - atakuwa dereva wa kwanza kukimbia katika kiwango cha juu hadi miaka ya 40 tangu bingwa wa dunia mara tatu Jack Brabham, ambaye alipata ushindi wake wa mwisho akiwa na umri wa miaka 44 mnamo 1970.

    Bingwa mara mbili Graham Hill aliendelea katika F1 hadi alipokuwa na umri wa miaka 46 mnamo 1975, ingawa tofauti na Alonso alitajwa kuwa aliyepita kiwango chake bora katika hatua za mwisho za taaluma yake.

  10. Rihanna: 'Nilikataa kununua nguo za ujauzito'

    j
    Image caption: Rihanna alivaa nywele za bandia za rangi ya dhahabu kwenye uzinduzi wa kiatu chake kipya cha Puma jijini London siku ya Jumatano

    Rihanna ameiambia BBC kuwa amefurahia kuandika upya sheria za mitindo kama mama, akisema "alikataa kununua nguo za ujauzito".

    "Nilijiambia ninataka kufanya kila kitu ninachofanya katika mitindo wangu ," alisema. "Nataka tu kufanya mambo kwa njia yangu na kila wakati nibadilishe na kuweka mtazamo wangu juu yake.

    "Nilifikiria nikasema nataka kuona kama chochote kinachofaa kitafanikiwa nitakifanya, na hiyo ilinifanya nijipe changamoto ya kuwa mjanga kwa mtindo," aliongeza.

    j
    Image caption: Rihanna, pichani akiwa na ujauzito wa mtoto wake wa kwanza mnamo 2022

    Alikuwa akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa ushirikiano wake hivu karibuni na kampuni ya mavazi ya Puma.

    Mshindi huyo wa tuzo nyingi za Grammy ana watoto wawili wa kiume na rapper A$AP Rocky - RZA Athelaston Mayers, aliyezaliwa mwaka wa 2022, na Riot Rose Mayers, aliyezaliwa mwaka wa 2023.

  11. Shughuli za binadamu zimechangia kuongezeka kwa kiwango cha joto Afrika

    h

    Mawimbi mabaya ya joto katika Afrika Magharibi na Sahel hayawezi kuisha bila mabadiliko ya hali ya hewa yaliyosababishwa na binadamu, wanasayansi wanasema.

    Halijoto imeongezeka na kufikia zaidi ya nyuzijoto 48C nchini Mali mwezi uliopita huku hospitali moja ikihusisha mamia ya vifo na joto kali.

    Watafiti wanasema shughuli za binadamu kama vile kuchoma mafuta zilisababisha ongezeko la nyuzijoto 1.4C na kuwa ya joto zaidi zaidi kuliko kawaida.

    Utafiti tofauti kuhusu ukame Kusini mwa Afŕika ulionyesha kuwa El Niño ndio ya kulaumiwa, badala ya mabadiliko ya hali ya hewa.

    Nchi kadhaa katika eneo la Sahel na Afrika Magharibi zilikumbwa na wimbi kali la joto lililopiga mwishoni mwa Machi na kudumu hadi mapema Aprili.

    Joto hilo lilikuwa la hali ya juu zaidi katika mikoa ya kusini ya Mali na Burkina Faso.

    Mjini Bamako, mji mkuu wa Mali, Hospitali ya Gabriel Toure ilisema ilirekodi vifo 102 katika siku za kwanza za mwezi Aprili.

    Karibu nusu ya watu waliokufa walikuwa na umri wa zaidi ya miaka 60, na hospitali ilisema kuwa joto lilichangiavingi ya vifo hivyo.

    Watafiti wanaamini kuwa mabadiliko ya hali ya hewa duniani yalikuwa na jukumu muhimu katika wimbi hili la joto la siku tano.

  12. Ujasusi wa Ujerumani: Washukiwa wawili wa upelelezi wakamatwa Bavaria

    g
    Image caption: Ujerumani ni nchi ya pili kwa kutoa misaada ya kijeshi kwa Ukraine baada ya Marekani

    Watu wawili wanaodaiwa kuwa majasusi wanaoshukiwa kupanga kuhujumu msaada wa kijeshi wa Ujerumani kwa Ukraine wamekamatwa katika jimbo la Bavaria kusini mwa Ujerumani.

    Wanaume hao wawili, walioelezewa kuwa ni raia wawili wa Ujerumani na Urusi, walizuiliwa huko Bayreuth kwa tuhuma za ujasusi wa Urusi, waendesha mashtaka wanasema.

    Dieter S, mwenye umri wa miaka 39, anashukiwa kwa msururu wa makosa ya ujasusi.

    Ni pamoja na kupanga njama za mlipuko, uchomaji moto na kudumisha mawasiliano na ujasusi wa Urusi.

    Pia anatuhumiwa kupigania jeshi la Urusi katika eneo la mashariki mwa Ukraine.

    Mshukiwa wa pili, aliyetambulika kwa jina la Alexander J, anatuhumiwa kumsaidia tangu mwezi uliopita kutambua watu wanaoweza kufanya mashambulizi. Anatakiwa kufika mahakamani siku ya Alhamisi.

    Ujerumani ni nchi ya pili kwa kutoa misaada ya kijeshi kwa Ukraine baada ya Marekani, ikitenga kiasi cha €28bn (£24bn) tangu kuanza kwa uvamizi kamili wa Urusi mwezi Februari, 2022.

  13. Israel ilitumia zaidi ya dola bilioni moja kuzuia mashambulizi ya Iran

    f
    Image caption: Iran ilifanya mashambulizi dhidi ya Israel, Aprili 14, 2024

    Gazeti la Yedhith Athronoth lilimnukuu kiongozi wa zamani wa kijeshi akisema kuwa Israel ilitumia zaidi ya shekeli bilioni 5 ( sawa na dola bilioni 1.35), usiku mmoja wakati wa kukabiliana na shambulizi lililoanzishwa na Iran dhidi ya Israel kwa kutumia ndege zisizo na rubani na makombora.

    Mshauri mkuu wa zamani wa majeshi ya Israel Ram Aminach, alisema kuwa shambulio la Iran liligharimu Israel kati ya shekeli bilioni 4 na bilioni 5 ( kati ya dola bilioni 1.08 na bilioni 1.35), na akaongeza kuwa gharama hizo zinahusu tu kukabiliana na ndege zisizokuwa na rubani na makombora kutoka Iran.

    h
    Image caption: Picha ya ndege ya kivita ya Israel ya F-15 baada ya misheni ya kuzuia shambulio la Iran

    Gharama hii haijumuishi hasara iliyopatikana kwenye uwanja,hasara ambayo jeshi la Israel liliitaja kuwa ni ndogo.

  14. Brazil: Mwanamke apeleka maiti benki ili kupata saini ya mkopo

    Mwanamke mmoja nchini Brazili amezua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii baada ya kupeleka maiti ya mzee katika benki, akitarajia kupata saini ya mkopo.

    Katika video iliyosambazwa mitandaoni mwanamke huyo alionekana akisukuma maiti ya mzee iliyekuwa imevishwa nguo nadhifu na kukalishwa kwenye kiti cha magurudumu hadi kwenye eneo la wateja kuhudumiwa na kujaribu kumfanya atie saini karatasi iliyokuwa mbele yake.

    Alimpa kalamu na kujaribu kumuita asaini karatasi hiyo lakini hakuweza kufanya hivyo.

    Wafanyakazi wa benki waliotilia shaka ustawi wa mwanamume huyo huko Rio de Janeiro walipiga simu polisi katika hatua iliyomfanya mwanamke huyo kukamatwa kwa madai ya ulaghai.

  15. Romario: Mshambulizi wa zamani wa Brazil ajiandikisha kuchezea klabu ya Soka ya Amerika pamoja na mwanawe

    .
    Image caption: Romario

    Mshambulizi wa zamani wa Brazil Romario ameacha kustaafu akiwa na umri wa miaka 58 na kusajiliwa kuchezea Klabu ya Soka ya Marekani pamoja na mwanawe.

    Romario, ambaye alishinda Kombe la Dunia la 1994, ni rais wa timu yenye maskani yake Rio de Janeiro, ambayo inacheza katika daraja la pili la mashindano ya kanda ya Rio.

    Romario alisema hatacheza ligi, lakini alitaka kushiriki katika baadhi ya michezo pamoja na mwanawe Romarinho.

    Romario alicheza mchezo wake wa mwisho mnamo Novemba 2009.

    Uchezaji wake ulianza mwaka 1985 akiwa na Vasco de Gama kabla ya kucheza vyema Uholanzi akiwa na PSV na Barcelona ya Uhispania.

    Alistaafu mnamo 2009, akicheza mchezo wake wa mwisho katika klabu ya Amerika FC, ambapo baba yake Edevair alicheza, kabla ya kuchaguliwa kuwa seneta wa Rio de Janeiro mnamo 2014.

    Alifunga mabao 55 katika mechi 70 alizoichezea Brazil, na alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Fifa mwaka wa 1994 baada ya kufunga mabao matano katika kampeni yao ya kushinda Kombe la Dunia.

  16. Juventus yaamriwa kumlipa Cristiano Ronaldo mshahara anaodai

    xx

    Klabu ya Juventus imeagizwa kumlipa Cristiano Ronaldo euro milioni 8.3 ambayo inadaiwa na mahakama ya Italia.

    Ronaldo, 39, alikubali kutochukua mshahara wake wakati soka nchini Italia liliposimamishwa na janga la Covid-19 msimu wa 2020-21

    Mreno huyo anadai klabu yake ya zamani zaidi ya euro milioni 17.

    Mahakama ya Usuluhishi wa mizozo ya michezo ilisema klabu hiyo inapaswa kulipa kile ambacho mchezaji huyo angepokea baada ya kukatwa kodi na makato mengine.

    Ronaldo alichezea Juventus nchini Italia kwa misimu mitatu kati ya 2018 na 2021, akiwasaidia kushinda mataji mawili ya Serie A.

    Aliondoka kwa kipindi chake cha pili akiwa na Manchester United na baada ya miezi 16 Old Trafford alijiunga na klabu ya Saudi Al-Nassr.

    Mshindi huyo mara tano wa taji la Ballon d'Or - aliyetunukiwa mchezaji bora wa dunia - aliorodheshwa na jarida la biashara la Marekani la Forbes kama mwanamichezo anayelipwa pesa nyingi zaidi mwaka wa 2023, akipokea mapato ya euro milioni 109.

  17. Ukraine yaonya kuhusu kutokea kwa vita vya tatu vya dunia

    xx

    Waziri mkuu wa Ukraine ameiambia BBC kutakuwa na "Vita vya Tatu vya Dunia" ikiwa Ukraine itashindwa katika mzozo kati yake na Urusi, huku akilitaka bunge la Marekani kupitisha mswada wa msaada wa kigeni uliokwama kwa muda mrefu.

    Denys Shmyhal alionyesha "matumaini makubwa" kwamba wabunge wa Marekani wangepitisha mswada huo unaokumbwa na mvutano mkali, ambayo inajumuisha dola bilioni 61 zilizotengwa kwa ajili ya Kyiv.

    Baraza la Wawakilishi linatazamiwa kupigia kura kifurushi hicho Jumamosi hii. Pendekezo hilo linajumuisha ufadhili kwa Israel pamoja na maeneo ya bahari ya Hindi na Pacific.

    Akizungumza na BBC mjini Washington DC siku ya Jumatano, Waziri Mkuu Shmyhal alisema kuhusu usaidizi wa usalama wa Marekani: "Tunahitaji pesa haraka iwezekanavyo." "Kama hatutalinda... Ukraine itaanguka," aliongeza.

    "Kwa hivyo mfumo wa usalama wa kimataifa utaharibiwa ... na ulimwengu wote utahitaji kupata ... mfumo mpya wa usalama. "Au, kutakuwa na migogoro mingi, aina nyingi za vita, na mwisho wa siku, inaweza kusababisha Vita vya Tatu vya Dunia."

    Hii si mara ya kwanza kwa Ukraine kutoa onyo hilo la kutisha kuhusu matokeo ya uwezekano wa kushindwa kwake.

    Maelezo zaidi:

    Je, Ukraine ina uwezo wa kuzuia mabomu ya kuongozwa ya Urusi

    Fahamu Ndege mpya za kivita za Urusi aina ya Su-57 na kwanini zinatumika kwa kificho?

    Je Ukraine kupewa ndege za kivita za F-16 kutaipa ushindi dhidi ya Urusi?

  18. Video: Tembo wa sarakasi azua sokomoko katika barabara baada ya kutoroka hifadhi

    Video content

    Video caption: Tembo mkaidi aliyetoroka hifadhi asababisha trafiki Montana

    Tembo aliyetoroka hifadhi amesababisha trafiki kubwa huko MontanaTembo huyo ambaye alikuwa akioshwakaribu na barabara, alishtushwa na sauti za magari, na akatoroka.

    Kanda za CCTV zilimuonesha akipita mbele ya magari kadhaa, na kisha kugeuka huku msimamizi wake akimfuata.

    Bill Melvin, meneja wa biashara wa eneo hilo, alisema tembo huyo alikuwa huru kwa takriban dakika 10 kabla ya kurejeshwa katika hifadhi hiyo.

  19. Askofu Australia aliyechomwa kisu kanisani amsamehe mshambuliaji wake

    Askofu Mar Mari Emmanuel
    Image caption: Askofu Mar Mari Emmanuel

    Askofu ambaye alichomwa kisu katika kanisa la Sydney siku ya Jumatatu amesema "naendelea kupata nafuu" na anamsamehe mtu anayedaiwa kumshambulia.

    Katika ujumbe wa sauti, Askofu Mar Mari Emmanuel pia aliitaka waumini kuwa watulivu.

    Polisi wanasema shambulio hilo ambalo lilirushwa moja kwa moja na ambalo lilisababisha watu wanne kujeruhiwa, lilikuwa ni kitendo cha kigaidi kilichochochewa na dini.

    Tukio hilo Ilizua ghasia nje ya Kanisa la The Good Shepherd, ambapo wafuasi wenye hasira wa askofu huyo walikuwa wamekusanyika.

    Mvulana mwenye umri wa miaka 16 - ambaye pia alijeruhiwa - amekamatwa kuhusiana na tukio hilo, lakini hajafunguliwa mashtaka yoyote.

    Mamlaka imekataa mara kwa mara kutaja imani zinazoshukiwa za mvulana huyo.

    Mapema wiki hii, mkuu wa Shirika la Ujasusi la Australia Mike Burgess alisema mamlaka inachunguza video ambazo zinadaiwa kumnasa mshukiwa akipiga kelele kwa Kiarabu na kurejelea neno "Nabii".

    Katika kanda ya dakika nne ya Askofu Emmanuel, iliyotolewa na kanisa kwenye mitandao ya kijamii siku ya Alhamisi, anasema amesamehe "yeyote aliyefanya kitendo hiki".

    "Nami nitawaombea ninyi daima. Na yeyote aliyewatuma kufanya hivyo, ninamsamehe pia katika jina kuu la Yesu," alisema.

  20. Rais wa Kenya atajwa miongoni mwa watu 100 wenye ushawishi duniani

    Rais wa Kenya William Ruto ndiye mwenyeji wa mkutano wa kilele wa hali ya hewa barani Afrika
    Image caption: Rais wa Kenya William Ruto mwaka jana alikuwa mwenyeji wa mkutano wa kilele wa hali ya hewa barani Afrika

    Jarida la Time limemtaka rais wa Kenya William Ruto kuwa miongoni mwa watu 100 walio na ushawishi mkubwa zaidi duniani mwaka wa 2024.

    Ruto aliibuka kama sauti kuu ya matarajio ya hali ya hewa ya Afrika na kutambuliwa kwa kuandaa mkutano wa kilele wa hali ya hewa mjini Nairobi Septemba mwaka jana, ambao uliwavutia viongozi kutoka kote ulimwenguni.

    Hafla hiyo ilihitimishwa kwa makubaliano ya pamoja kutoka kwa nchi za Afrika kupanua kwa haraka nishati mbadala katika muongo ujao, kwa kusaidiwa na dola bilioni 23 (Sh3 trilioni) katika ahadi za kuchochea malengo ya hali ya hewa ya bara.

    Jarida la Time lilitaja wito wa Ruto kwa wakopeshaji kupunguza mzigo wa madeni unaokabili baadhi ya nchi za Kiafrika, hivyo basi kufungua milango ya matumizi katika kutatua matatizo ya hali ya hewa kama jambo ambalo limeibua mjadala wenye tija.